Rc chalamila aagiza kufanyika uchunguzi haraka kubaini chanzo cha moto mwenge

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Decemba 05, 2023 amefika na kukagua athari zilizotokana na janga la moto katika eneo la Mwenge Wilaya ya Kinondoni usiku wa kuamkia leo ambapo fremu za wafanyabishara zaidi ya 30 zimeungua na moto huo.

RC Chalamila akiongea na wahanga wa moto huo ametoa pole kwa wote waliofikwa na janga hilo, ameagiza ufanyike uchunguzi wa haraka kubaini chanzo cha moto huo "kwa sasa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Kinondoni waangalie namna ya kuwasaidia wafanyabishara hao kwa kuwakopesha pesa ambayo watairudisha kwa riba kidogo ili waweze kuendelea na biashara kama awali" Alisema RC Chalamila

Aidha RC Chalamila amesema anatambua majanga hayo uweza kujitokeza kwa bahati mbaya, uzembe, au mipango ya watu wenye nia ovu hivyo uchunguzi ukikamilika hatua za kisheria zichukue mkondo wake

Vilevile Mhe Chalamila amewataka wananchi kutambua umuhimu wa matumizi ya Benki ili kuweka fedha zao na siko kuwa nazo dukani au nyumbani kutokana na janga hilo yako mabaki ya fedha zilizoungua hiyo ni ishara ya watu kukosa ufahamu wa Benki pia ametoa rai kwa wafanyabishara kuwa na bima ambayo itakuwa mkombozi nyakati za majanga.

Sambamba na hilo RC Chalamila ameagiza kufanyika maboresho ya fremu za maduka katika eneo hilo kwa kuwa Mwenge kwa sasa ni eneo muhimu kibiashara.

Kwa Upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Saad Mtambule amesema eneo hilo ni mali ya Bagdad lilikuwa na fremu 32, mali mbalimbali zimeungua, tayari timu ya uchunguzi imeundwa ikikamilisha kazi yake taarifa ya uchunguzi itawasilishwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, aidha ametoa shukrani kwa jeshi la polisi na wananchi waliojitokeza kuzima moto huo.

Share: