RAISI SAMIA AMPA WADHIFA MASAJU YA KUWA NDIO JAJI MKUU WA TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 13 Juni, 2025 amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. George Mcheche Masaju kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.

Uapisho wa Jaji Mkuu utafanyika June 15, 2025 Ikulu, Chamwino Dodoma kuanzia saa 4.00 asubuhi.


Itakumbukwa April 20,2023 Rais Samia alimteua Jaji George Masaju kuwa Mshauri wa Rais, Masuala ya Sheria (Advisor to the President - Legal Affairs) wakati huo Jaji Masaju alikuwa ni Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma.Baadaye January 10,2025 Rais Samia akafanya uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya Rufani wanne akiwemo Jaji George Mcheche Masaju ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu na Mshauri wa Rais, Sheria.


Mhe. Masaju alizaliwa tarehe 07 Aprili, 1965 katika Kijiji cha Bwai Wilaya ya Musoma mkoani Mara. Baada ya kuhitimu masomo katika ngazi mbalimbali za elimu ikiwemo Chuo Kikuu, aliajiriwa kuwa Wakili wa Serikali kuanzia mwezi Aprili, 1994 na kuendelea kufanya kazi hiyo hadi Oktoba, 2006.

  • George Mcheche Masaju ni Jaji Mkuu Mteule wa Tanzania, ambaye aliteuliwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mnamo tarehe 13 Juni 2025, kuchukua nafasi ya Prof. Ibrahim Hamis Juma aliyejistaafu. Uapisho wake rasmi unatarajiwa kufanyika tarehe 15 Juni 2025 katika Ikulu ya Chamwino, Dodoma .

Jaji Masaju amewahi kushika nyadhifa mbalimbali Serikalini. Aidha, kuanzia mwaka 2006 hadi 2009, Mhe. Masaju aliteuliwa kuwa Mshauri wa Rais wa Masuala ya Sheria na baadaye Oktoba, 2009 aliteuliwa kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, nafasi aliyohudumu hadi tarehe 02 Januari, 2015 alipoteuliwa na Rais wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.



Share: