Rais samia : vikwazo vya kibiashara vitaondolewa

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema wameazimia kuweka mazingira yatakayofanya biashara kati ya Tanzania na Zambia zisiwe na vikwazo. 

Wakiongea katika Kongamano la Wafanyabiashara wa Tanzania na Zambia nchini Zambia Marais hao wamesema eneo moja la muhimu ni kuhakikisha magari hayakai kwenye mipaka kwa muda mrefu pasi na sababu. 

Marais hao wanakutana kwenye mkutano wa ana kwa ana leo asubuhi na wamewaambia Wafanyabiashara hao kwamba mazungumzo yao yatajikita kwenye kuweka taratibu za kuondoa changamoto hizo.

Share: