Rais samia suluhu hassan amesema amesikitishwa na taarifa za kifo cha mtoto wa miaka miwili mwenye ualbino

Rais Samia Suluhu Hassan amesema amesikitishwa na taarifa za kifo cha Mtoto wa Miaka miwili mwenye Ualbino, Asiimwe Novath ambaye mwili wake ulipatikana jana Juni 17, 2024 baada ya kuchukuliwa na Watu ambao hawakufahamika akiwa nyumbani kwao Mei 30, 2024 katika Kijiji cha Bulamula, Wilayani Muleba Mkoani Kagera

Mwili huo umepatikana ukiwa umeondolewa baadhi ya viungo vyake ikiwemo Mikono, Ulimi na Macho

Rais Samia ametuma salamu zake za pole wakati akishiriki katika Kongamano la Maendeleo ya Sekta ya Habari, leo Juni 18, 2024 Jijini Dar es Salaam

Share: