Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Professa Kitila Mkumbo amesema moja ya watendaji muhimu ambao Rais Samia Suluhu Hassan amewapoteza ni aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Lawrence Nyasebwa Mafuru.
Prof. Kitila ameyasema hayo Novemba 10, alipokuwa amefika kutoa pole kwa familia ya Mafuru nyumbani kwake Bunju Dar Es Salaam ambapo ameeleza kuwa alikuwa ni mchapakazi mwenye nidhamu ya taaluma na mtendaji mwenye weledi katika nafasi yake.
Akielezea juu ya nyakati za mwisho za mawasiliano yake na Mafuru, Prof. Kitila amesema kuwa walisafiri pamoja yeye akielekea China ambapo walipofika Dubai waliachana ili Mafuru aelekee hospitalini. Na hata alipofika hospitali pindi alipopata nafuu ya kiafya alikuwa akishiriki katika vikao muhimu vya kuandaa na kujadili Rasimu ya Dira ya Taifa 2025-2050 huku akiwa kitandani.