Rais Samia Suluhu Hassan aagiza kufanyika ukaguzi wa majengo Kariakoo

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemuagiza waziri mkuu Kassim Majaliwa kuunda tume itakayofanya ukaguzi wa mejengo yote K/Koo kufuatia ajali iliyotokea ya ghorofa kuvunjika na kuleta mahafa makubwa kwa Tanzania.

Mhe.Rais amemtaka waziri mkuu kuunda tume hiyo ya ukaguzi itakayofanya kazi ya kukagua majengo yote yaliyopo K/Koo jijini Dar es salaam. Pamoja na hayo Mhe.Rais amelitaka jeshi la polisi kupata maelezo kutoka kwa mmiriki wa jengo lilivunjika kuhusu ujenzi wa ghorofa hilo.

Lakini pia Mhe.Rais ametaja idadi ya vifo vilivyothibitishwa mpaka sasa kuwa ni 13,mhe.rais amesema serikali itagharamia mazishi pamoja majeruhi wanaoendelea kupatiwa huduma.

Share: