RAIS MWINYI AWASILI JIJINI ARUSHA

lengo ni kuchunguza changamoto za tasnia ya habari uhuru wa vyombo vya habari, uchumi wa vyombo vya habari, umri wa miundo mbinu, na athari za mabadiliko ya tabianchi ....

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameondoka Zanzibar na Kuwasili Jijini Arusha kushiriki Mkutano wa Mabaraza huru ya Habari Afrika , unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).


Katika uwanja wa ndege wa Arusha amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha , Mhe.Kenani Laban Kihongosi na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Vyombo vya ulinzi na usalama wa Mkoa huo.


Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi, atahudhuria na kushiriki kwenye utoaji tuzo za miaka 30 ya MCT.

Mikutano ya kimataifa Ukiwemo mkutano huu inatarajiwa kuimarisha:

Udhibiti wa maudhui ya habari

Utumiaji wa teknolojia mpya kama AI katika vyombo vya habari

Uingiliaji wa kijinsia na watu wenye ulemavu katika habari

Itajumuisha maonyesho ya ICT, vyombo vya habari, taasisi za umma na sekta binafsi wakati wa kongamano .

Share: