Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye mkutano wa Waandishi wa Habari mara baada ya kushiriki Mjadala wa Kimataifa wa Norman E. Borlaung wenye lengo la kutatua changamoto ya upatikanaji wa chakula Duniani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye mkutano wa Waandishi wa Habari mara baada ya kushiriki Mjadala wa Kimataifa wa Norman E. Borlaung ambao uliandaliwa na Taasisi ya World Food Foundation katika Mji wa Des Moines, Iowa nchini Marekani tarehe 31 Oktoba, 2024. Mkutano huo unaowakutanisha wadau mbalimbali wa kilimo una lengo la kutafuta suluhu ya changamoto ya upatikanaji wa chakula Duniani inayochochewa na mabadiliko ya tabianchi.
Na pichani ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye Mjadala wa Kimataifa wa Norman E. Borlaung ambao uliandaliwa na Taasisi ya World Food Foundation katika Mji wa Des Moines, Iowa nchini Marekani tarehe 31 Oktoba, 2024. Kushoto ni Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina akimsikiliza. Rais Dkt. Samia ameelezea fursa mbalimbali za kilimo zinazopatikana Tanzania pamoja na hatua ya Serikali yake kuboresha Miundombinu ya usafirishaji ikiwemo Reli ya Kisasa (SGR) Bandari, masoko ya uhakika pamoja na mazingira mazuri kwa uwekezaji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Rais wa Sierra Leone Mhe. Julius Maada Bio kushoto pamoja na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina mara baada ya kushiriki Mjadala wa Kimataifa wa Norman E. Borlaung wenye lengo la kutafuta suluhu ya changamoto ya upatikanaji wa chakula Duniani inayochochewa na mabadiliko ya tabianchi. Mjadala huo umefanyika katika Mji wa Des Moines, Iowa nchini Marekani tarehe 31 Oktoba, 2024.