Rais ebrahim raisi pamoja na waziri wa mambo ya nje hossein amirabdollahian wameripotiwa kufariki katika ajali ya helikopta

 Rais Ebrahim Raisi pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amirabdollahian wameripotiwa kufariki katika ajali ya Helikopta iliyotokea katika eneo la Azerbaijan, Mashariki mwa Iran.


Taarifa zaidi kuhusu ajali hiyo zinaeleza kuwa Waokoaji wamefanikiwa kufika katika eneo la ajali lakini hadi kufika leo hakuna dalili ya kuwepo kwa walionusurika 

Kwa mujibu wa Katiba ya Iran, Makamu wa Rais, Muhammad Mukhbar anatarajiwa kushika nafasi ya Urais kwa muda wa Siku 50 wakati Nchi ikijiandaa kwa Uchaguzi wa Rais mpya


Share: