Rais dr. samia suluhu hassan ashiriki mjadala kuhusu kilimo barani Afrika

Rais Dr. Samia Suluhu Hassan Ashiriki mjadala kuhusu kilimo Barani Afrika

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Mtendaji Mkuu wa Millenium Challenge Corporation Bi. Alice Albright ambapo mazungumzo hayo yalijikita katika kukuza na kuimarisha mahusiano baina ya pande hizo mbili huko Des Moines, Lowa nchini Marekani.

Pichani ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki kwenye mjadala (round tables discussion )kuhusu kilimo barani Afrika, katika mji wa Des Moines, Lowa nchini Marekani tarehe 30 Oktoba, 2024. Mjadala huo ambao uliandaliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka barani Afrika, Serikali na Sekta binafsi ya Marekani hususani waliopo kwenye sekta ya kilimo.

Pichani ni Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akielezea Dira yake kuifanya Tanzania kuwa mzalishaji mkubwa zaidi wa chakula na kubainisha mikakati mikubwa mitatu ya Serikali katika kilimo. ameyasema hayo yote wakati akishiriki katika mjadala huo kuhusu kilimo barani Afrika, katika mji wa Des Moines, Lowa nchini Marekani  uliofanyika tarehe 30 Oktoba, 2024.

Pichani ni viongozi mbalimbali waliokuwa wakifuatilia mjadala huo kuhusu kilimo Barani Afrika katika mji wa Des Moines, Lowa nchini Marekani kando ya mjadala wa kimataifa wa Norman E. Borlaung ambao umeandaliwa na Taasisi ya World Food Foundation tarehe 30 Oktoba 2024.

Share: