Waziri wa nchi,ofisi ya Rais mipango na uwekezaji mhe Kitila mkumbo leo Januari 2, 2025 amezindua na kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari kainam yenye kidato cha tano na cha sita wenye thamani ya Shilingi millioni 428,9000
Akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe hilo la msingi waziri Kitila amesema lengo la mradi ni kuongeza miundombinu ya kidato cha tano na cha sita na kutoa nafasi kubwa ya wanafunzi wengi kuingia kidato cha tano na cha sita
Mkuu wa shule hiyo Emanuel Nikodemus wakati akieleza Maendeleo ya mradi huo amesema shule iyo ilipokea kiasi cha shilingi millioni 428,9000 mwezi mei, 2023 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili(2),madarasa sita(6) na matundu tisa ya vyoo ambapo matundu yaliyojengwa ni kumi(10)
Hata ivyo amebainisha jinsi mradi huo ulivyoleta manufaa kwa wanafunzi na wadau wa elimu shuleni hapo ambapo imesaidia kuongezeka kwa idadi kubwa ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita kutoka wanafunzi 44 hadi kufikia wanafunzi 612
Hii ni ziara ya kwanza ya waziri wa nchi ,ofisi ya Rais mipango na uwekezaji mhe. Prof Kitila Mkumbo mkoani Manyara kwa mwaka 2025 ambapo ataifanya kwa siku tatu(3) yenye lengo la kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya kimaendeleo katika mkoa huo.