Prof. katundu aridhishwa na ujenzi wa mradi wa maji nzuguni

Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Prof. Jamal Katundu ametembelea na kukagua maendeleo ya Mradi wa maji Nzuguni na kuridhishwa na kazi inayoendelea.

Aidha amejionea maandalizi ya uchimbaji wa kisima kikubwa kitakachokuwa na urefu wa mita 300 kwenda chini kitakachochibwa eneo Nzuguni pamoja na visima vingine vya kawaida vinavyoendelea kuchimbwa katika eneo hilo.

Pia ametembelea kituo cha kuzalisha na kusukuma maji cha Mzakwe na kujionea jinsi shughuli za uzalishaji zinavyofanyika.

Share: