Polisi watatu wafikishwa mahakamani wakidaiwa kuiba shilingi milioni 90.

Maofisa watatu wa Jeshi la Polisi wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za unyang'anyi wa kutumia silaha na kuiba shilingi milioni 90.

Washtakiwa hao ni Koplo Ramadhani (42) maarufu Rasta, Koplo Majid Abdallah (35) na Koplo Stella Mashaka (40). Wakili wa Serikali, Neema Moshi, aliwasomea washtakiwa hao shtaka moja la unyang'anyi linalowakabili, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Amir Msumi.

Alidai washtakiwa kwa pamoja Agosti 28, mwaka huu, maeneo ya Kurasini, jirani na Ofisi ya Uhamiaji, wilayani Temeke, waliiba shilingi milioni 90

Share: