Polisi wamewaua kwa kuwapiga risasi watu watano kenya, nairobi

Polisi katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, wamewaua kwa kuwapiga risasi risasi takriban watu watano wakati wa maandamano makubwa ya kupinga nyongeza ya kodi iliyopangwa, kulingana na Chama cha Madaktari cha Kenya.


Mwandishi wa habari wa shirika la habari la Reuters pia aliripoti kuhesabu miili ya waandamanaji watano nje ya bunge.

Hapo awali, umati wa watu ulivunja mstari wa ulinzi wa polisi na kuingia bungeni, na kuwasha moto katika sehemu ya eneo hilo.

Moto pia ulizuka katika Ukumbi wa Jiji la Nairobi,makao makuu ya kaunti hiyo.

Takriban watu 40 wanatibiwa hospitalini

Share: