Polisi ufaransa wamemkamata mwanamume mmoja kwa tuhuma za kujaribu kutengeneza vilipuzi

Polisi nchini Ufaransa wamemkamata mwanamume mwenye umri wa miaka 26 raia wa Urusi na Ukraine kwa tuhuma za kujaribu kutengeneza vilipuzi na kupanga kitendo cha vurugu.

Mwanamume huyo aliungua vibaya baada ya mlipuko kutokea Jumanne katika chumba cha hoteli huko Roissy-en-France, karibu na uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle mjini Paris.


Wachunguzi walipata ushahidi wa vifaa vilivyokusudiwa kutumiwa kutengenezea bomu kwenye chumba chake, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Kitaifa wa Kupambana na Ugaidi ilisema.

Bunduki na pasipoti za uwongo pia zilipatikana, kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya Ufaransa.

Waendesha mashtaka dhidi ya ugaidi wameanzisha uchunguzi.

Wanashirikiana na shirika la kijasusi la ndani la Ufaransa, chanzo kiliambia shirika la habari la Reuters.

Mtuhumiwa huyo kwa sasa anahojiwa hospitalini, baada ya kutibiwa majeraha ya moto na kisha kukamatwa.

Anaripotiwa kuwa mzungumzaji wa Kirusi kutoka eneo la Donbas mashariki mwa Ukraine, ambalo kwa sasa linakaliwa na Urusi.

Share: