PICHA ; SUNGU SUNGU NA BODA BODA WAPATA NAFASI MBELE YA RAIS SAMIA

Sungusungu pamoja na bodaboda kutoka mikoa ya Mwanza, Simiyu, Geita, Shinyanga na Tabora wamepata nafasi ya moja kwa moja mbele ya Rais wa Tanzania,Samia Amewapungia mkono na kuonesha dhairi anatambua umuhimu wa makundi hayo ....

Makundi mbalimbali ya walinzi wa jadi (Sungusungu) pamoja na bodaboda kutoka mikoa ya Mwanza, Simiyu, Geita, Shinyanga na Tabora yakipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza tarehe 20 Juni, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono walinzi wa jadi (Sungusungu) kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Geita na Tabora waliokuwa wakipita mbele ya jukwaa kuu katika uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza.


Share: