Paul makonda awataka Wajawazito kurudishiwa fedha walizolipishwa Simiyu

Mkazi wa Maswa Mkoani Simiyu, Monica Bona, amelalamikia kulipishwa gharama za afya kwa Wajawazito Wilayani hapo huku akisema anashangaa kuona wanalipishwa wakati Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameshatangaza kuwa Wajawazito wanatibiwa bure.

Akiongea mbele ya Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa, Paul Makonda, Monica amesema anazo risiti ambazo zinaonesha gharama alizolipishwa.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo amesema matibabu kwa Wajawazito ni bure na kwamba hakuwa na taarifa za kwamba kuna Watu wanalipishwa huku akiahidi kulifuatilia suala hilo na kama itabainika wamelipishwa Mama huyo na wengne waatarudishwa hela zao na hatua nyingine zitachukuliwa.

Share: