NYUMBA IMESHIKA MOTO ,WATOTO WA TATU WA FAMILIA MOJA WAFARIKI DUNIA

Watoto wa tatu wa familia moja wamekutwa wamefariki dunia baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi kushika moto.

Watoto hao wametambuliwa kwa majina ya Membe Ndama (7), Mwaru Ndama (2), na Sayi Ndama (1), ambao walikuwa wakiishi na wazazi wao katika Kijiji cha Nambilanje, Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi.


Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Lindi, John Imori, ambaye amesema kuwa janga hilo limetokea siku ya Jumatano majira ya saa 11:00 jioni.


Kwa mujibu wa Kamanda, nyumba hiyo ilikuwa na paa la makuti, jambo lililosababisha moto kuenea kwa haraka na kupelekea vifo vya watoto hao.

Aidha, Kamanda ametoa wito kwa wananchi kuepuka kuwaacha watoto peke yao majumbani bila uangalizi.

Share: