Nyumba 500 zimeathirika kigogo

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule amesema takribani nyumba 500 zimeathiriwa na mvua ambazo zimenyesha katika jiji la Dar es salaam jana November 12, 2023.

DC Mtambule amesema nyumba hizo zimezingirwa na maji ambayo yameingia ndani na kwa sasa jitihada mbalimbali zinafanyika kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ili kuhakikisha hakuna madhara zaidi yanatokea pamoja na kuona namna ya kurejesha mazingira ya kawaida.

Aidha DC Mtambule amesema miongoni mwa majengo ambayo yamezungukwa na maji ni pamoja na shule ya msingi Michael Urio.

Share: