Nigeria: wanafunzi 17 wa shule 5 wamepoteza maisha kutokana na mlipuko wa homa ya uti wa mgongo

2021 kulitokea mlipuko wa aina hiyo Nchini DRC na kuua zaidi ya Watu 129 ambapo Tanzania kupitia Ofisi ya Mganga Mkuu ilitoa tahadhari kwa Wananchi

Wanafunzi 17 wa Shule 5 katika Jimbo la Yobe wamepoteza maisha kutokana na mlipuko wa Homa ya Uti wa Mgongo (Meningitis), huku takwimu zikionesha kuna wengine 473 wanasumbuliwa na maradhi hayo.

Homa hiyo ni maambukizi ambayo husababisha kuvimba kwa tabaka za nje za Ubongo na Uti wa Mgongo na inaweza kuhatarisha maisha ya Mgonjwa kama haitatambulika mapema na kutibiwa huku Wataalam wa Afya wanaeleza kuwa chanjo ni njia bora ya kuzuia Ugonjwa huo.

2021 kulitokea mlipuko wa aina hiyo Nchini DRC na kuua zaidi ya Watu 129 ambapo Tanzania kupitia Ofisi ya Mganga Mkuu ilitoa tahadhari kwa Wananchi na kueleza Homa hiyo inasababishwa na vimelea aina ya Bakteria (Neisseria Meningitidis) wanaoambukizwa kwa njia ya hewa na inachukua Siku 2 hadi 10 tangu kuambukizwa hadi kuanza kuonesha dalili.

Share: