Nigeria: wahalifu wenye silaha waua watu 113

Makundi yenye silaha yameripotiwa kuua watu zaidi ya 100 katika mfululizo wa mashambulizi yaliyolenga miji ya katikati mwa Nigeria eneo lenye mivutano ya Kidini na Kikabila.

Uongozi wa Serikali ya Mtaa wa Bokkos, Jimbo la Plateau umeeleza mashambulizi hayo yamejeruhi zaidi ya Watu 300 na kuwa Serikali inafanya jitihada za kudhibiti mashambulizi hayo dhidi ya raia wasio na hatia.

Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International limesema Serikali imeshindwa kukomesha mashambulizi katika Jimbo la Plateau.

Hivi karibuni, Rais wa Nigeria, Bola Tinubu aliamuru uchunguzi ufanyike baada ya shambulizi la ndege zisizo na rubani kuwaua raia 85 waliokusanyika kwa ajili ya sherehe za kidini katika Jimbo hilo.

Share: