Ndejembi aipa maagizo tarura uyui

mkandarasi aliyepewa mradi huo mpaka sasa bado hajaanza kazi licha ya kuwa alishasaini mkataba wa ujenzi zaidi ya miezi mitatu iliyopita.

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Deogratius Ndejembi amemtaka Meneja wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Wilaya ya Uyui mkoani Tabora kuhakikisha mkandarasi aliyepewa kazi ya ujenzi wa barabara ya Ndevelwa-Igalula-Goweko anaanza kazi mara moja.

Mhe. Ndejembi ametoa agizo hilo katika Kijiji cha Igalula wilayani humo wakati akizindua Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Igalula, Mhe. Venant Protas ambapo Ofisi ya Rais-TAMISEMI ilipeleka kiasi cha Sh. Milioni Saba kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa ofisi hiyo.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Mhe. Ndejembi amesema amepokea malalamiko kwamba mkandarasi aliyepewa mradi huo mpaka sasa bado hajaanza kazi licha ya kuwa alishasaini mkataba wa ujenzi zaidi ya miezi mitatu iliyopita.

Share: