Shirika la ndege la Safarilink imesema kupitia mtandao wa X kwamba muda mfupi baada ya kupaa muda wa saa tatu na dakika 45 asubuhi
Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Kenya imethibitisha kisa cha kugongana kwa ndege ya abiria ya kampuni ya Safarilink na ndege ya mazoezi.
Uchunguzi umeanza kubaini chanzo cha ajili hiyo.
‘’Uchunguzi umeanza kupitia mashirika mbalimbali ukiongozwa na Idara ya Uchunguzi wa Ajali za Anga na Huduma ya Taifa ya Polisi kubaini chanzo cha ajali,’’ Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kenya imesema.
Abiria wawili waliokuwa kwenye ndege ya mazoezi wote wameaga dunia huku abiria 39 na wafanyakazi 5 katika ndege ya Safarilink wakiokolewa hadi eneo salama.
Shirika la ndege la Safarilink imesema kupitia mtandao wa X kwamba muda mfupi baada ya kupaa muda wa saa tatu na dakika 45 asubuhi saa za eneo hilo, kishindo kikubwa kimesikika.