Naira marley aachiwa huru

Msanii wa Nigeria Naira Marley, na meneja wake Sam Larry waachiwa kwa dhamana ya Naira milioni 20.

Mahakama ya Lagos iliyopo eneo la Yaba katika Jimbo hilo, ilitoa dhamana ya jumla ya Naira 20m kwa mwimbaji Azeez Fashola, anayejulikana zaidi kama Naira Marley na Balogun Eletu, maarufu kama Sam Larry.

Naira Marley, Sam Larry na wengine wawili walishtakiwa Oktoba 6 na kuwekwa rumande kwa kuhusishwa na mauaji ya mwimbaji, Ilerioluwa Aloba, anayejulikana kama Mohbad.

Hakimu aliamuru washtakiwa kukabidhi hati zao za kusafiria na kuripoti mara kwa mara kwenye Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai katika Jiji hilo.

Share: