Naibu waziri wa nishati mhe. kapinga akutana na uongozi wa tanesco.

Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga amekutana na Uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kuwaeleza kuwa wahakikishe wanamaliza changamoto sugu zinazowakabili wananchi.

Mhe. Judith amekutana na Uongozi huo Jijini Dodoma kwa lengo la kuzungumza nao na kufahamu namna walivyojipanga katika kutatua changamoto moto mbalimbali za umeme kwa wananchi.

Katika Mazungumzo yake, Mhe. Kapinga auelekeza Uongozi huo kuwahakikisha wanatatua changamoto sugu kwa kufanya kazi za ziada ili kuweza kupata mabadiliko katika utoaji wa huduma.

Amewataka kuweka mipango ya muda mrefu ili kumaliza changamoto ndogondogo akitolea mfano wa kukatika kwa umeme.

Pia amewataka kutatua kero zinazowakabili wananchi kwa wakati na kuzitolea ufafanuzi.

“Dunia imeendelea sana na teknolojia imekuwa mno, umeme kwa sasa si anasa hivyo kila mtu anahitaji huduma hiyo kwa matumizi ya aina mbalimbali, tuhakikishe tunawafikia wananchi ili waendane kulingana na Dunia ya sasa”, alisisitiza Mhe. Kapinga.

Kuongeza kasi ya kuunganisha wateja wapya na kuyafikishia huduma ya umeme maeneo ambayo bado hayajafikiwa na huduma hiyo.

Pia amewataka kuwashirikisha na kuwafahamisha viongozi wa Chama na Serikali wakiwemo Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Watendaji wa Serikali za Mitaa kuhusu miradi mbalimbali inayoendelea katika maeneo yao ili wafahamu vema na kuwaeleza wananchi wanaowaongoza.

Share: