Nachingwea waupiga mwingi kwa wahanga wa tembo

Harambee hiyo imewezesha kupatikana kwa mavazi, vyakula pamoja na fedha

Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani, Kamati ya wanawake wapenda maendeleo Wilaya Nachingwea chini ya Katibu wa Kamati hiyo Bi. Rose Msus Bi. Mariam Aden ambae ni Katibu wa ni Mhasibu wa Kamati hiyo wameandaa Harambee iliyofanyika jana February 26, 2024 katika ukumbi wa Mondlane Mess Wilayani Nachingwea kwa ajili ya kuchangia wahanga wa Tembo katika Kata za Nditi na Ngunichile.

Harambee hiyo imewezesha kupatikana kwa mavazi, vyakula pamoja na fedha taslimu Sh 2,780,000/= na ahadi ya Sh 2,534,000/= na kwafanya wanawake hao kuupiga mwingi kwa kuwa na jumla ya Sh 5,314,000/=

Mgeni rasmi wa harambee hiyo alikuwa ni Mkurugenzi Mendaji wa Halmashauri ya Nachingwea Mhandisi Chionda A. Kawawa. Wanawake wa makundi mbalimbali walijitokeza kufanikisha zoezi ili muhimu la kuwafuta machozi wakazi wa Ngunichile na Nditi.

Share: