Mgomo huo ulioanza leo Machi 11, 2024 umeripotiwa kusababisha usumbufu kwa baadhi ya abiria ambao wamesema umeathiri shughuli zao
Watoa Huduma za Usafiri wa Daladala wameingia katika Mgomo wakishinikiza Mamlaka kuzuia Bajaji walizodai zinaingilia safari na kuchukua abiria wao kwenye vituo vya daladala.
Wakizungumiza hatua hiyo, Wamiliki wa Daladala pamoja na Madereva wamesema kuna makubaliano yaliyowekwa awali juu ya utaoaji Huduma za Usafiri katika maeneo ya Jiji lakini yamekuwa hayafuatwi na Waendesha Bajaji na hivyo wanautaka Uongozi wa Mkoa kutafuta suluhu ya jambo hilo kwanza.
Mgomo huo ulioanza leo Machi 11, 2024 umeripotiwa kusababisha usumbufu kwa baadhi ya abiria ambao wamesema umeathiri shughuli zao ikiwemo kuchelewa katika majukumu yao kiasi cha kulazimika kutumia Babaji za mizigo huku wakilipa nauli kubwa.