Mwanajeshi wa israel adungwa kisu mjini jerusalem

Mwanajeshi wa Israel amejeruhiwa vibaya baada ya kudungwa kisu katika eneo la Jerusalem Mashariki linalokaliwa kwa mabavu, karibu na lango la Mji Mkongwe.

Mshambuaji anayeshukiwa kuwa na umri wa miaka 16 kutoka eneo la Issawiya mjini humo, amepigwa risasi na kuuawa na vikosi vya usalama baada ya kuwadunga kisu watu wawili kwenye mtaa wa Sultan Suleiman, polisi wa Israel wamesema.

Mshukiwa wa pili amekamatwa na uchunguzi unaendelea.

Huduma ya dharura ya Israel ya Magen David Adom (MDA), imethibitisha kuwa mwanamke mwenye umri wa miaka 20 amepelekwa hospitali kwa matibabu akiwa na majeraha mabaya.

Mtu wa pili pia alipata jeraha dogo la kuchomwa kisu katika shambulio hilo, ambalo MDA inasema kuwa lilifanyika karibu na lango la Mji Mkongwe wa Jerusalem.

Share: