Mwanajeshi nchini marekani apigwa risasi na kuuwa na polisi nyumbani kwake

Afisa aliyempiga risasi ambaye polisi hawajamtaja tangu wakati huo amepewa likizo.

Polisi huko Florida nchini Marekani wametoa hadharani picha za kamera kutoka kwa aliyempiga risasi mwanajeshi wa Jeshi la Wanahewa la Marekani nyumbani kwake.

Afisa mwandamizi katika jeshi la wanahewa Roger Fortson, ambaye alikuwa na umri wa miaka 23, alipelekwa hospitali ambapo alifariki, maafisa walisema.

Wakili wa familia ya mwathiriwa, akimnukuu shahidi, alidai polisi walivamia nyumba tofauti.



Hata hivyo, polisi wamepinga madai hayo na kusema naibu huyo alijibu kwa kujilinda baada ya kumuona Fortson akiwa amejihami kwa bunduki.

Mwanahewa huyo alipigwa risasi tarehe 3 Mei nyumbani kwake, iliyoko umbali wa maili 5 (8km) kutoka Mrengo wa Operesheni Maalum huko Hurlburt Field, Florida, anakoishi.

Afisa aliyempiga risasi ambaye polisi hawajamtaja tangu wakati huo amepewa likizo.

Afisa wa Kaunti ya Okaloosa Eric Aden alisema ufyatuaji risasi huo unachunguzwa na Idara ya Utekelezaji Sheria ya Florida na Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali.

Bw Aden aliahidi uwepo wa "uwazi na uwajibikaji" lakini akaongeza: "Uchunguzi huu unachukua muda."

"Lakini nataka kukuhakikishia kwamba hatujifichi, au hatuchukui hatua yoyote ambayo ingesababisha uamuzi wa haraka wa Bw Fortson au naibu wetu."

Afisa huyo alionyesha video ya dakika nne iliyochukuliwa kutoka kwa kamera iliyokuwa imevaliwa mwilini na naibu ambaye alifyatua risasi.

Share: