Mvua kubwa zitakumba maeneo ya dar, mafia, pemba, tanga, unguja na pwani

(TMA) imetoa tahadhari kwa raia waishio maeneo ya mabondeni pamoja na pembezoni mwa bahari kufwatia mvua za El Nino.

Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) imewataka Wakazi wa Dar, Tanga, Pwani, Mafia, Unguja na Pemba kuchukua tahadhari kutokana na maeneo hayo kutarajiwa kupata Mvua kubwa kuanzia leo Oktoba 29, 2023

TMA imeonya kuwa Mvua zitanyesha kwa siku 3 na zinaweza kubabisha Mafuriko pamoja na kuharibu shughuli za Kiuchumi hivyo Wananchi waepuke misongamano wa Watu, pia, wahifadhi mahitaji muhimu ndani. 

Awali TMA ilitabiri kuwa Tanzania inatarajia kukumbwa na Mvua za El Nino kuanzia Oktoba ambapo tayari Mikoa ya Tanga, Pemba na Unguja imeripotiwa kupata Mvua zinazozidi Milimita 50.

Share: