Mtwara: askari Wanne wa jeshi la wananchi tanzania (jwt) wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kulawiti

Amesema baada ya rufaa hiyo kusikilizwa April 03,2024 Mhakama Kuu ilibatilisha adhabu hiyo na kuwa kifungo cha miaka 30 jela

Aliyekuwa Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWT), Shaibu Yusuph Saidi (MT.95850) na wenzake watatu wamehukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kulawiti na kumpiga picha Mhanga wakati wakimlawiti huku wakimrekodi video na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Akitoa taarifa leo April 09,2024 kuhusu mafanikio ambayo Jeshi la Polisi limeyapata katika kesi zilizofikishwa Mahamamani katika kipindi cha January - March,2024, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara SACP Issa J.Suleiman amesema awali Watuhumiwa hao walihukumiwa kulipa faini ya Tsh. milioni moja katika Mahakama ya Wilaya ya Mtwara na baadaye upande wa Jamhuri walikata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara.

Amesema baada ya rufaa hiyo kusikilizwa April 03,2024 Mhakama Kuu ilibatilisha adhabu hiyo na kuwa kifungo cha miaka 30 jela na tayari Washtakiwa hao wameanza kutumikia adhabu yao.

Share: