Mtuhumiwa aliyemchoma mpenzi wake visu 25 akamatwa akijaribu kukimbilia kenya

Kijana Mkaazi wa Tarakea Rombo Mkoani Kilimanjaro Bw. Lucas Paul Tarimo amekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoaani Kilimanjaro alfajiri ya leo Dec 31 katika eneo la Geti la Ngorongoro baada ya kutaka kujaribu kukimbilia Nchi Jirani ya kenya.

Kijana huyo anatuhumiwa kwa kosa la kumchoma visu 25 katika maeneo mbalimbali ya mwili Binti aitwaye Beatrice James Minja(47) siku ya tarehe 12/11/2023 Rombo mkoani Kilimajaro.

Binti huyo ambae kwa sasa ni Marehemu, Taarifa zake zilianza kusambaa mitandaoni Nov 12 zikionyesha picha mbali mbali akiwa katika Hospitali ya KCMC ambazo ziliibua hisia kali hadi kupelekea Jeshi la Polisi kutoa Taarifa za kuanza msako wa kumtafuta mtuhumiwa.

Taarifa iliyotolewa leo Dec 31, 2023 na Jeshi la polisi inaeleza jitahada za jeshi hilo na ushirikiano wa wananchi uliopelekea kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo ambae alijaribu kunywa sumu ya kuulia wadudu lakini aliwahiwa na kwa sasa yuko Mikononi mwa polisi akisubiri taratibu zingine zikamilike afikishwe Mahakani.

Share: