Mtuhumiwa aliyemchoma mpenzi wake visu 25 afariki dunia baada ya kukamatwa na polisi

Mtuhumiwa wa Mauaji ya Beatrice Minja Bw. Lucas Paul Tarimo amefariki Dunia kutokana na Sumu ya wadudu inayosadikiwa alikunywa muda mfupi baada ya kuwaona Polisi waliokua wanamtafuta.

Katika Taarifa iliyotolewa awali na Jeshi la Polisi ilieleza kukamatwa kwa Bw. Tarimo alfajiri ya Dec 31 huko Ngorongoro huku akiwa amekutwa na Sumu aliyokua ameanza kuinywa kwa dhamira ya kujiua.

Beatrice Minja alifariki katika Hospitali ya KCMC baada ya kuuguza majeraha yaliyotaka na kuchomwa visu 25 na Bw. Tarimo huku chanzo cha Tukio hilo kikiwa hakijaelezwa.

Marehemu Paul Lucas Tarimo alimchoma visu 25 anayesadikiwa kuwa ni mpenzi wake Beatrice Minja siku ya Nov 12 2023 huko Rombo mkoani Kilimanjaro, naye kukamatwa katika kijiji cha Jema wilayani Ngorongoro akijaribu kukimbia kuelekea Nchi Jirani ya Kenya.

Share: