Mrembo mtalii abakwa na wanaume 7 mbele ya mume wake

Mwanamke mwenye umri wa miaka 28 raia wa hispania na mumewe walivamiwa na genge la wahuni na mwanamke huyo alibakwa na watu 7 mbele ya mumewe huko Jharkhand India.

Wapenzi hao ambao wanatumia pikipiki kuzunguka dunia walikuwa wameweka hema lao kwa ajili ya kupumzika siku ya Ijumaa usiku na ndipo tukio hilo likatokea

Polisi walisema walikamata wanaume watatu na walikuwa wakiwasaka wengine wanne kuhusiana na ubakaji wa mwanamke huyo raia wa Uhispania na shambulio la mume wake mwenye umri wa miaka 64.

Share: