Mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya Billion 2 wazinduliwa Babati

Waziri wa nchi ofisi ya Rais mipango na uwekezaji mhe. prof Kitila Mkumbo leo Januari 4, 2025 amezindua na kuweka jiwe la msingi kwenye mradi mkubwa wa maji uliopo katika kata ya Arri halmshauri ya wilaya ya babati vijijini unaotajwa kugharimu shilingi billioni 2,610,938,015

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa maradi huo prof Kitila amesema moja ya adhima ya serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ni 'kumtua mama ndoo ya maji kichwani' hivyo ni furaha kubwa kuona mradi huo umekamilika na unaenda kuwahudumia wakazi wa kata ya Arri wenye vijiji zaidi ya saba

Sambamba na hilo prof Kitila amewasifu na kuwashukuru wadau wa maendelo (shirika la karimu) kusaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha kukamilika kwa skimu hiyo ya maji kwani wamechangia zaidi ya billioni 2 hivyo kuharakisha kukamilika kwa mradi huo



Kwa upande wake Daniel Sillo naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi na mbunge wa jimbo la babati vijijini amewashukuru wananchi kwa kujitoa kuchimba mitaro,kulaza mabomba na kufukia mitaro ya maji kwani wamechangia kwa kiasi kikubwa kukamilika kwa mradi huo ambao unakwenda kumaliza tatizo la maji lililodumu kwa muda mrefu kwenye zaidi ya vijiji sita ambavyo ni Managha,Dudiye,Dohom,Endasago,Arri,Sharmo na Tsaayo


Share: