Mr beast azikwa akiwa mzima siku 7

Staa wa youtube MrBeast amejirecord video akiwa amezikwa hai kwa siku saba. Video Iliopata views milioni 57 saa chache baada ya kupostiwa youtube, na kuibua mijadala kwenye mitandao ya kijamii, na ilipostiwa kusherehekea hatua yake muhimu ya kuwa na wafuasi milioni 200.

Katika video yake ya hivi punde, ‘I Spent 7 Days Buried Alive’, MrBeast, alijirekodi kuzikwa kwenye kaburi la futi sita kwa siku saba. Ili kujiandaa kwa tukio lake jipya zaidi, MrBeast alipanga kaburi la muda na jeneza la kioo chini ya ardhi. Mara tu alipoingia kwenye jeneza, gari la ujenzi liliweka mchanga ndani ya shamba hilo hadi likafunikwa kabisa, na MrBeast alisema ni jambo la kutisha zaidi ambalo amefanya, kama ilivyoripotiwa na MEAWW.

Akiwa kwenye jeneza, alieleza jinsi atakavyoishi kwa siku saba kwa kuonyesha mkoba uliokuwa na MREs na vitafunwa. Zaidi ya hayo, aliwaambia watazamaji wake kwamba watu watatu walikuwa wakifuatilia hali yake kila mara ikiwa mambo yataenda kombo, MrBeast alikuwa akihisi uchovu sana siku ya nne na akasema hakuweza kulala.

Share: