Mmoja aswekwa rumande njama za kushambulia kanisa ujerumani

Polisi nchini Ujerumani imesema imemweka rumande mwanaume mmoja anayeshukiwa kupanga njama za kufanya shambulio kwenye kanisa kuu mjini Cologne wakati wa mkesha wa mwaka mpya.

Hata hivyo hapo jana wanne kati yao waliachiwa huru na polisi imesema mmoja atabakia rumande kama sehemu ya hatua muhimu ya "kuepusha kutokea balaa". Hati ya mahakama imetoa kibali kwa mwanaume huyo aliyetambulishwa kwa jina moja la Tajik kuwekwa kizuizi hadi mnamo Januari 7.

Polisi imesema inatumia njia zote zilizopo kuepusha kutokea kisa chenye madhara kwa umma na kulilinda kanisa la mjini Cologne ambalo ni moja ya majengo ya kale kabisa barani Ulaya na tunu nchini Ujerumani

Share: