Mkuu wa wilaya ya bariadi simalenga anadaiwa kuwafukuza waandishi wa habari kwenye kikao cha ushauri

Taarifa ya Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani humo (SMPC) imesema Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Simon Simalenga, anadaiwa kuwafukuza Waandishi kwa dhihaka kwenye kikao cha Ushauri cha Wilaya kilichofanyika Februari 19, 2024

Taarifa imesema licha ya kitendo hicho kuwafedhehesha Waandishi na tasnia ya Habari, rekodi zinaonesha hiyo siyo mara ya kwanza kwa Kiongozi huyo kufanya hivyo, ambapo mara ya kwanza aliwatolea maneno ya kudhalilisha Mwenyekiti na Makamu wa SMPC

Aidha, Klabu imetoa wito kwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kutoa tamko juu ya tukio hilo. 

Share: