Meya kumbilamoto achanja mbuga kutatua kero za wananchi

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Mhe Omary Kumbilamoto amekabidhi mifuko Saba ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa kivuko cha watembea kwa miguu kwenye moja ya eneo lililopo mtaa wa Kombo kata ya Vingunguti.

Ikumbukwe huo ni muendelezo wa kutatua kero zinazozowakabili wananchi wa kata hiyo ikiwa ni ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM inayotaka kuhakiki viongozi wanawatumikia wananchi kwa kutatua kero zao.

Mpaka sasa vimekamilika vivuko viwili kati ya vitano anavyojenga kwenye mtaa huo

Share: