Mchungaji lamor whitehead wa brooklyn amehukumiwa kifungo cha miaka tisa jela

Maafisa wanasema Whitehead aliwahadaa watu kwa ahadi za uwongo na kuwaibia pesa zao kununua vitu vikiwemo mavazi ya kifahari na magari.

Mchungaji mmoja mtanashati wa Brooklyn amehukumiwa kifungo cha miaka tisa jela kwa makosa ambayo ni pamoja na kupora akaunti ya benki ya mmoja wa wafuasi wake.

Lamor Whitehead, mhubiri wa New York maarufu sana kutokana na maisha yake ya kifahari, alipatikana na hatia mnamo Machi kwa makosa ya ulaghai kwa njia ya mawasiliano ya kielektroniki, kujaribu unyang'anyi na kutoa taarifa za uwongo kwa wapelelzi.

Waendesha mashtaka walidai kuwa Whitehead, 45, alitumia nafasi yake kama kiongozi wa kidini kuwahadaa watu pesa ili kugharamia maisha yake ya kifahari.

Whitehead aligonga vichwa vya habari mnamo 2022 baada ya kuibiwa akiwa ameelekezewa bunduki wakati wa mahubiri yaliyotiririshwa moja kwa moja.


Wezi hao walifanikiwa kupata $1m (£840,000) gharama ya saa, almasi na zumaridi.

Damian Williams, Mwanasheria alimuita Whitehead "mtu mdanganyifu" na kusema kwamba hukumu hiyo inaashiria mwisho wa "mipango yake mbalimbali".

Maafisa wanasema Whitehead aliwahadaa watu kwa ahadi za uwongo na kuwaibia pesa zao kununua vitu vikiwemo mavazi ya kifahari na magari.

Mmoja wa waathirika, mshiriki wa kanisa lake, alimpa $90,000, akiba yake akiamini kwamba pesa hizo zingeenda kumnunulia nyumba.

Badala yake ilitumika kwa malipo ya nguo na gari.

Pia alithibitisha hati ili kupata mikopo ya biashara na alijaribu kumnyang'anya mfanyabiashara wa mji wa Bronx kwa kudai kwa uwongo kuwa na uwezo wa kumfikia Meya wa New York Eric Adams.

"Askofu Whitehead yuko katika maombi yangu," meya alisema Jumatatu kabla ya hukumu, kulingana na New York Times. Mawakili wa Whitehead walisema wanapanga kupambana dhidi ya hukumu yake.

Share: