Mwaka uliopita, visa 9,000 vya watu kuvamiwa na mbwa viliripotiwa nchini Msumbiji, ambayo ilikuwa ongezeko la 21% kutoka 2022.
Baadhi Mataifa ya Afrika yakiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Msumbiji, yamepiga marufuku baadhi ya mbwa kufuatia mashambulizi na ongezeko la visa vya mbwa hao kuwavamia watu.
Rais wa DRC Felix Tshisekedi ameitaka serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani na Wizara ya Afya, Usafi kudhibiti umiliki wa aina ya mbwa fulani, pit bulls na boerboels kutokana na “kuenea kwa wasiwasi” wa mbwa hao kuwashambulia watu.
Msemaji wa Serikali Patrick Muyaya amesema kuwa jambo hilo linatia wasiwasi zaidi kwani mbwa hao, “huhifadhiwa na idadi ya vijana ambao hawajui hatari au athari ya mbwa hao.”
Mapema mwezi huu, Msumbiji ilipiga marufuku uagizaji wa aina 23 ya mbwa ikiwemo pitbulls, boerboels, na rottweilers.
Mwaka uliopita, visa 9,000 vya watu kuvamiwa na mbwa viliripotiwa nchini Msumbiji, ambayo ilikuwa ongezeko la 21% kutoka 2022.