Mashalovie yupo hatiani kuswekwa ndani, unatafutwa ushahidi tu

Mashalovie yupo hatiani kuswekwa ndani unatafutwa ushahidi tu

Waziri Wa Maendeleo Ya Jamii,Jinsia,Wanawake Na Wenye Mahitaji Maalumu Dorothy Gwajima Amewataka Watu Kumtumia Ushahidi Kwenye Tuhuma Ambazo Amekua Akitagiwa Na Nawatu Kua Mashalove Nimoja Ya Watu Wanaochangia Kuharibu Maadili Kwenye Jamii 

Waziri Gwajima Ameandika haya:- "Ndugu wana jamii, salaam. Ahsanteni Sana kwa ushirikiano wa kuniletea kila taarifa inayohusu matendo ya kuchochea mmomonyoko wa maadili. Hata hivyo, peke yangu mimi bila nyie siwezi, maana hawa ni watoto wetu majumbani kwetu.

Haya, hii picha ni kutoka kipande cha video kinachosikika kikitangaza biashara niseme ya ukahaba huko kunakoitwa 'LIQUID BAR'. Video hii WENGI MNAIJUA maana IMEZUNGUKA SANA na nimetumiwa mara kadhaa.

Sasa,

1. Wahusika wa video hii na tangazo hilo, mna leseni ya biashara hii mnayotangaza? Maana huwa hakuna leseni ya mambo haya yaliyo kinyume na maadili, hivyo hakuna uhalali wa Tangazo hili.

2. Nyie mabinti mnaojitangaza, ni sehemu ya wanawake ambao kila siku tunalia tunanyanyaswa tunahitaji kuheshimiwa kwa sheria kali kali: itawezekanaje wakati sisi ndiyo tuna promote mkao wa kukatiliwa?

3. Kama ni biashara halali, mbona inawezakana kupitia mikopo ya wanawake tunayotangaza kila siku. Shida ni hatujui au uvivu na kutaka hela za haraka haraka?

WITO; Kwanza msitishe hili jambo ambalo awali ni kinyume na Sheria zote, kisha nakuja huko mje mniambie shida nini hadi mnafikia hali hii kwenye nyakati hizi zenye fursa za kutosha kufanya biashara halali....... Katika kuja kwangu huko, nawasiliana na MKUU WENU WA WILAYA kwanza.....

TUACHE KUJIDHALILISHA WENYEWE na kufungua milango ya kudhalilishwa na wengine. TUTUMIE FURSA HALALI ZA MAENDELEO YA JAMII.

Pia akaongezea kwakumuulizia mashalove ambaye inasadikika ndiye aliyehusika na kurekodi tangazo hilo kwakusema :-

"Kwani huyu mashalove ambaye kila siku mnamtaja taja humu link yake Iko wapi tuone yaliyomo? Maana Kila mtu humu mashalove mashalove..... Na wengine ni akina nani hao ambao tunasema waache mambo ya kuchochea mmomonyoko wa maadili wao hawasikii la mwalimu wala la daktari? Na huku sheria tunazo........

Komenti ziwe fupi fupi, usindikize na ushahidi na kama ushahidi huo ni mbaya njoo DM kabla hawajafuta link .. download, screenshot pia..... MKAKATI ni tuwape mamlaka husika wafanye Kazi zao........"

Share: