maafisa wa usalama wamesema uhalifu huo umefanywa na "magaidi wa kigeni". Saa chache baadaye, kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu IS lilidai kuhusika
Marekani imelaani "shambulio la kutisha la kigaidi" lililotokea wakati wa misa ya Kikatoliki katika chuo kikuu kwenye mji wa Marawi kusini mwa Ufilipino ambapo watu wanne wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Washington imesema inafanya mawasiliano ya karibu na mshirika wake Ufilipino.
Msemaji wa kituo cha polisi huko Lanao del Sur Meja Alinaid Moner, ameviambia vyombo vya habari leo hii kuwa wanaendelea na doria na kwamba usalama umeimarishwa shuleni hapo na kusisitiza kuwa Chuo Kikuu cha Jimbo la Mindanao (MSU) kinaendelea na shughuli zake kama kawaida.
Awali, rais wa Ufilipino Ferdinand Marcos Jr na maafisa wa usalama wamesema uhalifu huo umefanywa na "magaidi wa kigeni". Saa chache baadaye, kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu IS lilidai kuhusika na shambulio la bomu katika ukumbi wa mazoezi wa chuo hicho.