Marekani: vipande vya kuku vyatakiwa kurejeshwa baada ya kupatikana na mabaki ya chuma

Wasindikaji wa nyama wa Marekani wa kampuni ya Tyson Foods wanasema wametangaza kurejeshwa kwa takribani 30,000lbs (13,608kg) za vipande vya kuku, baada ya mabaki ya chuma kupatikana katika bidhaa hiyo.

Kampuni hiyo ilisema wito wa kurejesha bidhaa hiyo ni "kutokana na tahadhari ya juu".

Bidhaa hiyo ilitengenezwa katika kituo kimoja na kusafirishwa kwa wasambazaji katika majimbo tisa ya Marekani ikiwa ni pamoja na Alabama, California na Illinois.

Huduma ya Usalama na Ukaguzi wa Chakula ya Marekani (FSIS) ilisema imepokea ripoti moja ya jeraha dogo la mdomo.

FSIS ilisema mtu yeyote mwenye wasiwasi wa jeraha au ugonjwa anapaswa kuwasiliana na mtoa huduma ya afya.

Bidhaa hiyo yenye umbo la dinosaur iliyoathiriwa na wito wa kurejeshwa ina muda wa kutumika hadi tarehe 4 Septemba 2024.

Share: