Marekani: Rapa P. Diddy afunguliwa mashtaka mapya ya unyanyasaji wa kingono

Rapa Mkongwe, Mtayarishaji wa Muziki na Mfanyabiashara, Sean Combs "Diddy" amefunguliwa mashtaka mengine ya Unyanyasaji Kingono na Joi Dickerson-Neal ambaye amemtuhumu Diddy kuwa alimpa Dawa za Kulevya na kumdhalilisha Kingono, Januari 3, 1991

Joi anadai baada ya kupewa Dawa na kudhalilishwa, aligundua Diddy au Puff Daddy au P. Diddy alirekodi tukio hilo kwa siri na kuwaonesha watu kadhaa

Mwanasheria wa Diddy amedai tuhuma hizo ni za kutunga na mlalamikaji ana nia ya kujipatia fedha. Ikumbukwe siku kadhaa zilizopita Diddy alifunguliwa mashitaka kama hayo na aliyekuwa mpenzi wake "Cassie" lakini baadaye walimalizana nje ya Mahakama.

Share: