Maporomoko ya ardhi yaua watu 47 manyara

Takriban watu 47 wamekufa na wengine 85 wamejeruhiwa kufuatia maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mafuriko katika mkoa wa Manyara. 

Hayo yameelezwa jana usiku na mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga huku akionya kuwa idadi hiyo huenda ikaongezeka.

Mkuu wa wilaya Janeth Mayanja amesema mvua kubwa ilinyesha Jumamosi katika mji wa Katesh, karibu kilomita 300 kaskazini mwa mji mkuu Dodoma. Mayanja ameongeza kuwa barabara nyingi katika eneo hilo zimezuiliwa na udongo, miti na mawe vilisombwa na mafuriko hayo.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akihudhuria mkutano wa Umoja wa mataifa wa hali ya hewa wa COP28, ametuma salamu za rambirambi na kusema ameagiza kuwepo " juhudi zaidi za serikali ili kuokoa maisha ya watu".

Share: