Mama wa miaka 70 ajifungua mapacha uganda

Mwanamke wa Uganda mwenye umri wa miaka 70 amepata mapacha baada ya kupata ujauzito kupitia matibabu ya kupandikiza (IVF) na kuwa Mwanamke Mzee zaidi barani Afrika kujifungua, kwa mujibu wa Hospitali alikopata watoto.

Kituo cha Kimataifa cha Hospitali ya Wanawake a Kituo cha Uzazi katika Mji Mkuu wa Uganda, Kampala, kimesema Safina Namukwaya alijifungua Mtoto wa kike na wa kiume kwa njia ya upasuaji. 

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Hospitali hiyo imesema “Hadithi hii haihusu tu mafanikio ya matibabu inahusu nguvu na uthabiti wa roho ya Mwanadamu”

Share: