Malawi: kanisa katoliki limemkosoa rais lazarus chakwera

Kanisa Katoliki lenye ushawishi mkubwa nchini Malawi limemkosoa Rais Lazarus Chakwera, likisema nchi imekuwa mbaya zaidi katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake.

Katika kaulinzito inayoonekana kuelekezwa kwa rais, kanisa hilo kupitia maaskofu wake lilisema "tumeshuhudia kufeli kwa uongozi".

"Raia wa Malawi hawaoni mtu yeyote katika serikali ya sasa anayewajali au ambaye anaweza kuboresha hali zao," iliongeza.

Waraka wa wachungaji wenye kurasa 16 wenye kichwa "Hadithi ya kusikitisha ya Malawi", iliyosomwa katika makanisa yote ya Kikatoliki nchini kote siku ya Jumapili, ulishutumu uongozi kwa kushindwa kwa kiasi kikubwa kutekelezwa ahadi za kampeni, upendeleo wa kindugu na ufisadi uliokithiri.

Kanisa hilo linashutumu serikali ya Bw Chakwera kwa kupendelea watu wa kabila au eneo fulani inapowateua watu kwenye nyadhifa za juu na kuwadhulumu wanahabari wanaofichua ufisadi.

Waraka huo pia ulisema serikali imeshindwa kuinua kipato cha watu hata baada thamani sarafu ya Malawi kushuka kwa kiasi kikubwa.

Share: