Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, amemuomba Mkuu wa Mkoa mpya, Kenani Kihongosi, kuhakikisha anaendeleza ndoto ya kuufanya Mkoa wa Arusha kuwa na hadhi ya Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).


 Repoter : ‎Gladness Kowero, Arusha

‎Makonda alitoa kauli hiyo wakati wa hafla ya makabidhiano ya ofisi yaliyofanyika jijini Arusha, ambapo alieleza kuwa ana imani na uongozi wa Kihongosi kuwa ataendeleza mipango na maono aliyoyaacha.

‎“Ninaamini kuwa Kihongosi ataendeleza yale yote tuliyoyaanzisha, hususani dhamira ya kulifanya Jiji la Arusha kuwa mfano wa Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki,” amesema Makonda.