MAKALA ; MBIO NA MKESHA WA MWENGE WA HURU ZAFANA SANA DAR ES SALAAM

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 Awataka Vijana Kuwa Wazalendo katika Kujenga Taifa Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2025, Ndugu Ismail Ali Usi, amewataka vijana wa Tanzania kuwa wazalendo wa kweli katika kulijenga taifa, akisisitiza kuwa uzalendo ni miongoni mwa tunu muhimu ya taifa letu.Dar es salaam mbio hizi zimetimua vumbi.Kauli mbiu "“Jitokeze kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu”

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU KITAIFA BW. ISMAIL ALI USSI, LEO JUNI 03, 2025 AMEWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA MRADI WA TENKI LA MAJI - BAGULO, HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM

Mkuu wa wilaya ya Ilala Mheshimiwa Edward Mpogolo @mpogoloe ameupokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe.Halima Bulembo ambapo Mwenge huu unatarajiwa kutembelea,kukagua na kuweka jiwe la msingi miradi 7 yenye jumla ya Shilingi bilioni 44.3.

Wilaya ya Ilala mwenge umekesha na wananchi wameitikia wito kwakishindo huku burudani mbali mbali ikiwemo burudani ya maonesho ya muziki ilifanyika huku jukwaa la mkesha wa mwemge kusheheni wasanii wengi tofauti akiwemo super star Diamond ,MC Balaa , Chino wana Man , nawengine kibao wakikonga moyo mashabiki  ndani ya uwanja wa chuo cha kampala ,ilala Gongo la mboto.


Share: